Scalp ni ngozi ya kichwa na hivyo ina tabia kama ya ngozi ya sehemu nyingine za mwili. Kama vile mtu anavokua na dead skin (ngozi iliyokufa usoni) ndio hivyo hivyo anaweza kuwa na dead skin kichwani pia. Ngozi ya kichwa ikizidiwa uchafu iwe kwa sababu ya kuto kuosha nywele vizuri au kuganda kwa mafuta au products nyingine za nywele na kutengeneza kitu kinaitwa Product build up (Pitia post No. 31 & 32) au dead cells kuziba hair roots na kushindwa kuzalisha ngozi mpya ni lazima ukuaji wa nywele zako ufifie.

SCALP EXFOLIATION
Hii inahusisha kutumia njia mbali mbali kuondoa dead skin kichwani, mafuta yaliyoganga (au extra sebum) na mba. Ni muhimu sana katika utunzaji wa nywele uwe na tamaduni ya kufanya scrub ya kichwa ili kupata nywele zenye afya, imara kuanzia kwenye shina na zinazong'aa vizuri. Leo tutaangalia njia rahisi sana ya kufanya scalp exfoliation nyumbani. Ni rahisi, nzuri na inatumia gharama kidogo.

MAHITAJI
-Sukari (natural /brown sugar) vijiko viwili vya chakula
-Kijiko kimoja cha mafuta  (Pure castor oil/coconut oil or olive oil)
-1/2 Apple cider vinegar au Limao
-Scalp massager
-Gloves (ukipenda)

JINSI YA KUTUMIA
-Saga sukari kwa blender au twanga kwa kinu kidogo cha viungo
-Changanya vyote upate kama paste hivi (scrub)
-Tumia vidole vyako au brash (scalp massager) kumassage ngozi ya kichwa ili kufanya scalp relaxation.
-Osha nywele vizuri kwa sulphate free shampoo
-Nywele zikiwa bado zina maji maji kidogo, kata mstari paka scrub kidogo
-Massage scalp yako taratibu kwa dakika 5-10 (tumia scalp massager au vidole)
-Fanya ivyo kwa kichwa kizima
-Baada ya kumaliza osha vizuri kwa maji ya baridi hadi uhakikishe hakuna particles za sukari zilizobaki.
-Baada ya hapo fuata LOC Method (leave in conditioner, oils, cream-shear butter)
-Halafu unaweza suka nywele za uzi (African threading method) ili kunyoosha nywele zako.

USITUMIE MOTO KUNYOOSHA NYWELE ZAKO

NB: Maji ya baridi husaidia kutunza mafuta ya asili kichwani (sebum)