Mba ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wengi na kusababisha kuwepo kwa vipande vidogo vidogo vyeupe vya ngozi kama ukurutu, ambavyo huweza kukudhalilisha, kuwasha na kuuma muda mwingine. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa matunzo mazuri ya ngozi na kichwa.
☘️Kisayansi, kawaida ngozi hujimenya seli za ngozi ziliyozeeka, na hizi seli hupotea bila kugundulika. Vipande vidogo vya mba vinasababishwa na ongezeko la seli za ngozi katika kichwa, ongezeko hili husababisha pia ongezeko la seli za ngozi zilizozeeka kutolewa. Seli hizi zikikutana na mafuta kwenye nywele na kichwa, pamoja zinaonekana na kufanya mba. Mba huchangia sana kukatika kwa nywele na kufanya nywele zisiwe na afya nzuri au kukua vzr.
UTAGUNDUAJE KUWA UNA MBA
Kubanduka kwa ngozi ya kichwa kwa kasi(Kubanduka huku kuna ambatana na kuwashwa kwa ngozi ya kichwa, ambapo inapelekea kuwepo kwa vipande vidogo vidogo vyeupe vya ngozi(ukurutu) kwenye kichwa, nywele na mabega.
AINA ZA MBA KICHWANI
Kuna aina mbili za mba katika kichwa:
🍀Mba wa kawaida/ wastani aina hii inaweza kutibika kwa matumizi ya shampoo, na tiba asili za kutengeneza nyumbani kama vile mafuta ya nazi na juice ya alovera, castor oil, juice ya limao n.k
☘️Mba mkali au uliokithiri, aina hii ya mba katika kichwa inaambatana na kuwashwa kwa kichwa, kuvimba na uwepo wa mba wenye urefu sawa na nywele za kichwani. Mba katika hatua hii unaweza kutibika kwa dawa zilizoshauriwaa na wataalamu wa afya.
MBA UNASABABISHWA NA NINI?
Hakuna chanzo maalumu kinachojulikana cha mba katika kichwa, ila zipo sababu ambazo zinatajwa na watu kuwa vyanzo vya mba kichwani. Miongoni mwa visababishi vya mba katika kichwa ni kama:
✨Uchafu: usafi duni wa kichwa na nywele ni moja ya sababu za kuwa na mba kichwani, ni vema kusafisha kichwa na nywele mara tatu mpaka nne kwa wiki au mara moja kwa wiki kama nywele zako ni ndefu
✨Kutumia mafuta ya mgando kichwani ambayo yanapelekea kuganda kichwani na kuleta mba
✨Pia unapokwangua mba ndio unapozidi kutapakaa au kusambaa
🌿Vyanzo vingine vya mba kichwani vinatajwa kuwa:
✨Utumiaji wa vipodozi vya nywele sana kama vile gelly za kulainisha nywele.
✨Kuwa na ngozi kavu sana kichwani (spray mchanganyiko wa maji na mafuta kila inapobidi)
✨Kutumia vitu kama chanuo, brash, kitana pamoja na mtu mwenye mba
✨Utumiaji wa hali ya juu wa “chlorinated swimmimg pools”.
✨Utumiaji wa bidhaa zenye chumvi au maji ya chumvi kwenye nywele
MATIBABU YA MBA KICHWANI
☘️Mba unaweza kupotea ghafla bila matibabu au unaweza kuhitaji kutunza kichwa na nywele kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu. Mara nyingine mba katika kichwa unaweza kuchukua wiki nyingi kutibika. Baadhi ya matibabu ya mba wa kichwani yanaweza kuwa ya tiba asili au tiba ya kisasa.
🍀Inashauriwa zaidi kutumia tiba ya asili kutibu mba wa kichwani, mojawapo wa tiba hizo za asili ni kama:
✨Mafuta ya nazi original na juice ya kutengeneza ya alovera. Juisi ya alovera inatumika pamoja na shampoo ya kuosha kichwa na nywele na mafuta ya nazi kwaajili ya kulainisha ngozi na nywele.
✨Juice ya limao, juice ya limao ina citric acid inayoweza kushambulia fangasi zinazosababisha ukurutu wa ngozi ya kichwa na pia inasaidia kupandisha juu ngozi zilizokufa juu na kuweza kuzisafisha kwa urahisi.
NB: Kamua limao na upate juice ambayo itatumika kusugua kichwani kisha suuza na maji,fanya hivi kila ukitaka kuosha nywele.
✨Castor oil original (paka kila asubuhi kwenye ngozi ya kichwa iliyo safi)
UTAJIKINGA VIPI USIPATE MBA
Ni vema kchukua hatua ili kuzuia mba kichwani ili usifikie hatua ya hatari zaidi, Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kufuatwa ili kupunguza au kutokomeza kabisa mba kichwani:
☘️Kula kawaida, mlo wenye afya ulio jumuisha matunda na mbogamboga kwa wingi. Punguza vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi kwa wingi.
☘️Safisha kichwa na nywele zako walau mara tatu mpaka nne kwa wiki au mara moja kama nywele zako ni ndefu na suuza kwa maji mengi.
☘️Epuka vitu vyenye chemicals nyingi kwenye nywele (Tumia vitu vya asili kwa nywele zako kama mafuta ya kupika nyumbani ya nazi, juice ya aloevera, castor oil au juice ya limao kutibu nywele zako).
Post a Comment
Post a Comment