Katika Post No. 58 tulijifunza jinsi ya kutumia majani ya mpera kama leave in conditioner, pamoja na faida zake kadhaa. Majani ya mpera (guava leaves) ni kati ya kiungo muhimu sana ambacho watu wengi wanaotumza nywele zao kimewaletea matokeo chanya sana. Hivyo hata wewe msomaji kama bado hujajaribu unatakiwa kujaribu iwe ni kuzipa nywele zako unyevu au kama chakula cha nywele.

FAIDA ZA MAJANI YA MPERA 
-Yanafanya nywele zinakua laini
-Yanarudisha rangi ya asili ya nywele na kung’aa zaidi
-Kujaza nywele 
-Nywele zinakua well moisturized

MAHITAJI
-Majani kadhaa ya mpera (10 hadi 20 yanatosha kabisa)
-Mafuta ya maji (Castor oil, coconut or olive oil)
-Asali kiasi

JINSI YA KUANDAA
-Safisha majani yako vizuri ili kuondoa uchafu na takataka zote.
-Yaweke majani kwenye blender na ongeza maji kidogo halafu blend ili kupata juice
-Chuja vizuri mchanganyiko wako ili kupata juice safi
-Ongeza mafuta kidogo na asali kidogo tu (kulingana na kiasi cha juice yako)
-Baada ya kuosha nywele vizuri na shampoo paka steaming yako kichwa kizima kuanzia kwemye shina la nywele
-Baada ya hapo vaa kofia ya plastic au kaa kwenye steamer ili joto liingie vizuri na kufanya steaming iingie vizuri kwenye nywele
-Baada ya dk 45 hadi 1 hour osha nywele zako vizuri kwa maji ya baridi.
-Ukimaliza paka mafuta yako vizuri na Cream (shear butter) halafu unaweza suka style yoyote unayoipenda.