Scalp kama ilivozoeleka ni ngozi ya kichwa ambayo ndio inapokea nywele changa kabisa kutoka ndani. Scalp massage ina umuhimu sana katika ukuaji wa nywele na hata katika afya kiujumla japo wengi wamekua wakiipuuzia hii step katika utunzaji wa nywele. Scalp massage tunaifanya ili kupunguza tension, kuleta utulivu wa mawazo (relaxation) na kuleta wepesi wa kichwa. Hii inafanyika ukiwa umesuka, umebana nywele au hata ukiwa umeaschia.

JINSI YA KUFANYA
-Paka mafuta kwenye ngozi ya kichwa na kwenye mikono yako
-Sugua taratibu kichwani huku ukiwa umeinamia chini kama inawezekana (hii inachochea mzunguko wa damu kwenye nerves za kichwa) kwa muda wa dk 5.
-Siku ya kuosha nywele (HAIR WASH DAY) unaweza fanya massage na mafuta yako (carrier oils-castor oil, jojoba oil, coconut oil etc) kwa muda wa dk 3 halafu yaache kwenye nywele kwa muda wa dk 15-30 kabla ya kuosha nywele kwa shampoo au conditioner (hii inaitwa PREPOO)

UMUHIMU WA KUFANYA SCALP MASSAGE
-Ngozi ya kichwa ikirelax hata ukuaji wa nywele unakua kama invotakiwa na sio wa kusuasua.
-Ina hamasisha mzunguko mzuri wa damu kichwani
-Inasaidia kulainisha nywele na kufanya products ziingie vizuri na kufanya kazi vizuri
-Inasaidia kuimarisha shina la nywele (hair strands/roots)
-Inasaidia kulainisha ngozi ya kichwa
-Husaidia kuweka balance ya mafuta kichwani (Natural scalp sebum)
-Inasaidia kupata usingizi vizuri , kupunguza uchovu na maumivu ya kichwa.

NB: Hakikisha unakua na utaratibu wa kufanya scalp massage kila unapopaka hair product yoyote au unapofanya treatment yoyote ya nywele angalau kwa dakika tano tu at least mara tatu kwa wiki. Hii inafanyika kwa wanawake, wanaume na watoto pia.