kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa yanayowekwa kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika, kukosa afya pamoja na mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako kiusahihi zaidi.
🧚🏻♂️Kata ncha za nywele zako
kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. Seli zinapokufa huzuia nywele zinazozaliwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. Japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.
🧚🏻♂️Osha nywele zako angalau mara moja kwa wiki
Kuosha nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya na safi; hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuziosha nywele zako.
🧚🏻♂️Tumia shampoo inayoendana na nywele zako
Tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu, nzito nk.. Zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo, hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.
🧚🏻♂️Zipe nywele zako nafasi
Nywele nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku, kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya, hivyo unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kupumzika na kupumua kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu.
🧚🏻♂️Usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.
Jaribu kuzichana nywele kwa chanuo kubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibu ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.
🧚🏻♂️Zilinde nywele zako unapokuwa unaogelea
Unapokua unaogelea baharini au kwenye bwawa la kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzuia zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe nywele zako kwa maji safi na uzikaushe.
🧚🏻♂️Kula vyakula venye protein na matunda kwa wingi
kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimarisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.
🧚🏻♂️Zifunge nywele zako kabla ya kulala
Unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifunga vizuri na kuzibana. Kulala huku ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika
🧚🏻♂️Tumia mafuta asili
Badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. Tumia mafuta kama ya mnyonyo au nazi au parachichi kupaka nywele zako.
🧚🏻♂️Zilimde nywele zako na jua
Wakati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. pia unaweza kuzipaka sunscreen.
Post a Comment
Post a Comment