HAYA NI MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
kuchagua uweke dawa gani ya box au ya kopo hutegemea na ngozi yako ya kichwa kama iko sensitive yaani inaungua haraka unashauriwa dawa ya box,na wenye ngozi ambayo sio sensitive yaani haiungui haraka mnashauriwa kuweka dawa ya kopo au yoyote utakayoipenda wewe.
Dawa zimegawanyika makundi matatu
🧚🏻♂️Regular/normal
🧚🏻♂️Super/extra
🧚🏻♂️Mild
Hii mild siku hizi haipo na hapa tutazungumzia dawa mbili tu regural ambayo jina lingine ni normal na super ambayo jina lingine ni extra .
Unashauriwa kuangalia kopo au box lako kujua unatumia dawa gani sio kujiwekea tu ilimradi hlf unataka kuwa na nywele nzuri.
MATUMIZI
🧚🏻♂️Normal /regular hii ni dawa ambayo unashauriwa utumie mtu mwenye fine na medium hair yaani mtu mwenye nywele laini na zisizo ngumu wala laini zipo kati
🧚🏻♂️Extra hii inatumika for course hair,yaani nywele ngumu
NB: Ijue nywele yako ni ya aina gani usijipakie dawa tu, kuna watu wanalalamika nywele haishiki dawa ni ngumu kumbe anapaka dawa ya watu wenye nywele laini normal badala ya kupaka extra,na mwenye nywele laini anapaka super za watu wenye nywele ngumu utaishia kulia nywele nyepesi zinanyonyoka kumbe tatizo ni lako.
MAMBO YA KUZUNGATIA
🧚🏻♂️Zingatiab muda wa kukaa na dawa kichwani; Usizidishe wala kupunguza bali fuata maelekezo ya muda wa kukaa nayo huwa wanaanddika kwenye box na kopo.
🧚🏻♂️Muda wa kuretouch inafuatana na jinsi nywele zilivyoota muda wa chini wa kufanya retouch ni wiki 10-12 na kuendelea usiwahi chini ya hapo kwani zilizootea zitakuwa chache ukizidi weka dawa nywele ambayo haijaotea hukatika
🧚🏻♂️Paka dawa nywele iliyoota tu usiguse yenye dawa,upake chini tu.
🧚🏻♂️Ukimaliza kuweka dawa jitahidi kufanya steaming(deep conditioner)
🧚🏻♂️Kuwa na mazoea ya kusoma,product kilichoandikwa usikurupuke.
🧚🏻♂️Zipende nywele zako na zielewe zinataka nini.
Ukifuata mambo hayo utazipenda nywele zako tofauti na wengine wanavozichukia nywele zao za dawa.
Post a Comment
Post a Comment