Hii ni moja ya vitu ambavyo watu wengi wanaotunza nywele zao wanateseka navyo na wengi bado hawajajua solution ni nini. Wengi wanalalamika kuwa na nywele kavu, kuuma wakti wanachana, kukatika nk. Sasa leo tuangalie vitu unavyotakiwa kufanya ili nywele zisikakamae au kuwa kavu, zisiume wakati wa kuchana na kukatika.
VITU VYA KUFANYA
🧚♀️DEEP CONDITIONING (STEAMING)
Hii ni solution ya kwanza , kufanya steaming nywele zako mara kwa mara inasaidia sana. Kila kampuni yenye products za Natural hair inakua na shampoo/ conditioner /moisturizer / detangler nk kulingana na matumizi yako. Ni muhimu sana kuchagua products/bidhaa zenye ubora kulingana na nywele zako (usiangalie gharama ila angalia ubora).
Hivyo basi kama wewe una nywele kavu. baada tu ya kuosha lazima upake conditioner ili kulainisha nywele zako at list mara moja kwa wiki au kila unapoisha nywele zako.
🧚♀️ KUVAA KOFIA YA SATINI/KUFUNGA KITAMBAA CHA SATINI/ KUTUMIA MTO WENYE FORONYA YA SATUNI ULALAPO
Hii inasaidia sana kutunza unyevu unyevu (kuwa moisturized) maana usipovaa usipofanya hivyo itakua ngumu kutunza unyevu nyevu wa nywele. Najua inakera kulala umejibana kichwaa ila furaha huwa zaidi asubuhi utapoamka huku nywele zako zikiwa laini na sio kavu na pia inazuia usumbufu pamoja na kuchafua foronya nyingine na mafuta ya nywele. Hii pia inapunguza nafasi kubwa ya nywele kukatika.
🧚♀️KUBADILI BRAND / PRODUCT UNAYOTUMIA
Yes ni kweli ulishauriwa na muuzaji au uliisoma online ina review nzuri au ulikutakana na mdada mwenye natural hair ambaye alikupa ushirikiano ulipomuuliza anatumia product gani ya nywele akakujibu nawe ukaenda nunua ukaanza itumia, lakini sio kila product inamfaa kila mtu kwa sababu ya utofauti wa aina ya nywele; Hivyo ukiwa umetumia hair product kwa muda na huoni matokeo ni muda wa kuachana nayo na kujaribu nyingine mpaka nywele zako zitakapokubali ndio utabaki na hiyo.
🧚♀️PUNGUZA MIONZI YA KUZIPASI AU KUNYOOSHA NYWELE (ACHA KUTUMIA MOTO)
Ni kawaida sana siku ukitaka kubadili muonekano au hair style ukaamua kuzichoma/kusipasi au kunyoosha nywele zako kwa kutumia moto (umeme). Unashauriwa kupunguza temperature au kutumia kinga (mafuta maalum) ambayo inafanya nywele zako zisipate damage wakati ya kuzinyoosha hii itakusaidia kutunza moisture sambamba na kupunguza ukatikaji wa nywele zako.
🧚♀️MAJI NDANI NA NJE
Yes huwezi pinga hili maji ndio kila kitu kwa afya ya mwili na hata maisha ya kila siku. Unatakiwa kunywa maji meengi uwezavyo na pia unatakiwa kutumia products hasa Leave in Conditioner ambazo ni WATER BASED PRODUCTS. Na pia maji ndo product isiyo ya bei ghali na iliyo rahisi kupatikana na kuitumia. Hivyo kunywa maji mengi uwezavyo na kunyunyizia maji kwenye nywele zako.
Post a Comment
Post a Comment