STEAMING YA KITUNGUU
Mahitaji
🍃Vitunguu maji (vyekundu) vikubwa vitatu (3)
🍃Vitunguu swaumu punje 5
🍃Limao au ndimu moja kubwa
🍃Tangawizi (moja ndogo)
🍃Mafuta ya castor oil (kijiko kimoja)
🍃Mafuta ya nazi na olive oil (kijiko kimoja)
🍃Asali kijiko kimoja
JINSI YA KUANDAA
🌿Menya vitunguu maji na swaumu na uvikate kate vipande vidogovidogo.
🌿Andaa tangawizi pia zioshe na kuzimenya.
🌿Changanya vyote, kamulia na ndimu au limao pamoja na asali na usage katika blender vyote upate juice nzito kidogo.
🌿Chuja vizuri kwa kutumia chujio au kitambaa kuondoa makapi na hakikisha umeichuja vizuri.
🌿Chukua juice uliyoiandaa changanya na mafuta yako ya Castor oil, ya nazi na olive oil ichanyanyike vizuri.
🌿Hapa nywele zako zikiwa tayari safi (umeshaisha kwa shampoo) waweza tumia kitambaa cha cotton au pamba unaaza kujipaka kwanzia kwenye Ngozi kuja kwenye nywele (hapa yahitaji uvumilivu maana utaona kama harufu ya pilau kdg kichwani)
🌿Vaa shower cap au steamer kaa kwa dk 50+ kisha osha vizuri bila shampoo mpaka uhakikishe zile nywele harufu inaisha
🌿Tumia tisht au kitambaa cha cotton kukausha nywele yako (usitumie taulo maana linakata nywele)
🌿Waweza tengeneza gel ya bamia utumie kama leave in conditioner (Angalia post inayofata)
🌿Paka vizuri gel yako tayari kwa kubana au kusuka🔥🔥😍😍
NB: Steaming hii inasaidia vitu vingi ikiwepo;
🍃Kuondoa mba na miwasho
🍃Kujaza nywele
🍃Kuzifanya nywele ziwe laini
🍃Kuimarisha mizizi ya nywele
🍃Kutibu vidonda vilivyosababishwa na kujikuna kichwani
Post a Comment
Post a Comment