Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi na nywele.
🍃Yanalainisha  na kung’arisha nywele zako.
🍃Yanajaza nywele kwa sababu ya Amino acid inayopatikana kwenye maji ya mchele.
🍃Yanaimarisha nywele na kufungua vitundu vya ngozi (hair pores ) ili ziweze kukua vizuri.
🍃Kuondoa  miwasho na mba kichwani
🍃Kujaza nywele


JINSI YA KUANDAA
✨Andaa mchele wako robo kilo (1/4 kg - mchele aina yoyote)
✨Osha vizuri kisha weka kwenye sufuria yako safi.
✨Ongeza maji mengi au kadiria zaidi ya hapo  mchele ulipoishia maana unafyonza maji sana.
✨Weka jikoni na ufunike.
✨Acha uchemke kwa dakika 10  hivi kwa moto wa wastani (usiive) au hadi uone mchele unaanza kulainika kwa mbali.
✨Epua na uache upoe kidogo kisha chuja na kitambaa au chujio safi.
✨Weka kwenye kopo maji uliyoyachuja na ufunike vizuri usiku mzima, asubuhi ongeza maji kikombe kimoja ili kupunguza nguvu.

NB: Unaweza kutengeneza zaidi ukahifadhi kwenye friji kwa wiki mbili.

NAMNA YA KUTUMIA
✨Fanya pree poo kama kawaida ya Alovera au hot oil treatment (Ntaelekeza kwenye post inayofata)
✨Shampoo nywele zako (Paka shampoo kwenye ngozi ya kichwa, lowanisha na sugua vizuri ngozi pamoja na nywele zako)
✨Suuza na maji ya mchele na ufunike kichwa kwa dakika 30.(utasuuza na maji ya kawaida baada ya hizo dakika)
✨Fanya deep conditioning kwa dakika 30 (yoyote uliyo nayo)
✨Suuza tena nywele zako na maji ya kawaida
✨Kisha pakaa leave in conditioner yako, mafuta yako uyapendayo kwenye nywele (tumia mafuta ya maji) kwa sababu mafuta ya mgando yanaleta mba na kumalizia na cream (shea butter)
✨Style nywele zako ulivyozoea au nenda kasuke