FAIDA ZA TUI LA NAZI KWEYE NYWELE
Mahitaji
🍃Nazi moja iliyokomaa vizuri
🍃Unga wa pilipili manga nyeusi
🍃Unga wa mbegu za uwatu (fenugreek)
Jinsi ya kuandaa
🌿Kuna nazi yako vizuri kwa kutumia mbuzi au mashine
🌿Tengeneza tui lako zito kidogo ukitumia nazi uliyokuna
NB: Ili kupata tui zito na jingi nakushauri ukisha kuna nazi yako iweke kwenye blender na maji kidogo kwa mbali kisha blend kwa dakika kadhaa ndipo ukamuwe upate tui zito kabisa na jingi.
🌿Mimina tui hilo kwenye sufuria na uweke kwenye moto kama dakika 3 au 4 kustimulate nutrients kwa kuwa litakaa kwenye nywele muda mfupi
🌿Subiri tui hilo lipowe na mwisho pakaa kichwani kichwa chote au sehemu ambayo nywele zimepotea na uache hivyo kama dakika 20 hadi 30 (kama steaming au protein treatments nyingine)
🌿 Safisha kichwa na nywele zako kwa kutumia mild shampoo (Isiyo na sulfate au chumvi au viambata vingine vyote vyenye sumu).
Faida za tui la nazi kwenye nywele
🌿Tui la nazi lina kiasi kingi cha protein na mafuta mengine muhimu ambavyo huhamasisha ukuaji wa nywele
🌿Husaidia uotaji wa nywele na hivyo kuzuia kipara pia.
🌿Tui la nazi likipakwa mara kwa mara kwenye nywele halikawii kuleta matokeo mazuri.
🌿Hujaza nywele
🌿Kufanya nywele kuwa nyeusi na kujaa
MUHIMU
Kufanya tui liwe na nguvu zaidi unaweza kuongeza vitu vifuatavyo;
🌸Kijiko kimoja cha chai cha unga wa pilipili manga nyeusi
🌸 Kiasi hicho hicho cha unga wa mbegu za uwatu (Fenugreek)
Post a Comment
Post a Comment