🧚🏽‍♂️Wengi wetu tunapenda urembo, lakini kwa bahati nzuri au mbaya wa afrika tume barikiwa na nywele ngumu hii imetupelekea kupenda kuweka dawa za nywele ili kuzilainisha na kuzipa muoneko mzuri, lakini dawa hizi zina uzuri na ubaya wake.


🥵Sayansi inaonyesha kuwa matumizi ya relaxer za nywele yanaweza kusababisha au kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya;

-Moyo

-Kupungua kwa uwezo wa kiakili katika kufikiri na kupambanua mambo -Kuungua kwa ngozi ya kichwa 

-Muwasho wa ngozi.


🥵Matatizo mengine ni; -Saratani ya matiti -Mabonge katika mji wa mimba (Leiomyomata) -Upungufu wa kinga ya mwili

-Kubalehe mapema kwa wasichana. 


🌿Mabonge yanaweza kusababisha ugumba hasa pale yanapokuwa makubwa na kulazimisha tiba ya upasuaji ya kuondoa kizazi (hysterectomy). 


NB: Katika jamii za wanawake wanaotumia relaxer kwa kiwango kikubwa, chanzo kikubwa cha upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi ni mabonge.


🌿Inasemekana kuwa katika nchi ya Marekani wanawake weusi wanakabiliwa na tatizo la mabonge mara mbili hadi mara tatu zaidi ya wanawake wengine. Hii inaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na matumizi makubwa ya vipodozi kama relaxer.

Viambato vilivyomo ndani ya dawa hii hupenya na kuingia katika mfumo wa damu na kwenda kuvuruga mfumo wa vichocheo vya ujinsia hasa homoni za kike. Relaxer nyingi za nywele zina kiwango kikubwa cha kemikali kama vile;

-Lye (Sodium hydroxide au Caustic soda)

-Calcium hydroxide -Guanidine carbonate -Thioglycolic acid 

-Salts 

-Monobutyl phthalate.