*SEALING MOISTURE/KUZIPA NYWELE UNYEVU*

Hii ni process ya kulock in Moisture/ kufungia unyevu kwenye nywele ili usipotee.

🌺Lakin siku zote kabla ya kufanya sealing hakikisha umespray/umenyunyiza nywele na maji hasa hasa ukiwa unatumia butters kama Shea butter

Yani usijaribu kupaka shea butter kwenye nywele kavu


🌺Unafanya sealing kwenye hair strands/mzizi wa nywele kwa kutumia mafuta mazito au hair butters 

Hii inaaongeza extra layer ya ulinzi kwenye nywele zako ili zikae na unyevu kwa muda mrefu na nina amini wote tumeshajua umuhimu wa nywele kuwa na moisture.

Ukipaka shea butter nywele zikiwa kavu hutoona hata hiyo sealing effect au ability ya shea butter kuseal na kulainisha nywele zako.


-Halafu wakati wa kufanya sealing in ukifika kwenye ncha inatakiwa kuwa makini zaidi, maana nywele inakatika juu kwenye ncha, kwa hiyo ukiwa unafanya sealing hakikisha your ends ( ncha) are well moisturized (zimepata unyevu wa kutosha) na ikibidi ongeza hata kiasi cha butter unachotumia.


JINSI YA KUSEAL IN MOISTURE

1. Nyunyizia nywele maji, kidogo tu lakini usilowanishe nywele kabisaa kwa urahisi zaidi tumia spray bottle.

2.Halafu paka mafuta yako sasa kama ni coconut oil/mafuta ya nazi, olive au jojoba (mafuta yoyote ya kimiminika ambayo ni mepesi).

3. Halafu sasa pakaa hair butter ambayo ndio main sealing oil.

: Kwahiyo hapo step ni Maji halafu mafuta na mwisho ni Butter.


🌺ENJOY YOUR NATURAL HAIR🌺