Wote tunajua katika jamii zetu muarobaini/neem ni dawa nzuri sana ya asili, lakini leo sitakngelea kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali ya mwili; Ila nitaongelea jinsi gani muarobaini unaweza tumika katika kukuza nywele zetu (hasa nywele za asili).

FAIDA ZA MUAROBAINI KWENYW NYWELE
🧚🏻‍♂️Ni anti-bacterial; Na hii huenda kwenye scalp moja kwa moja hivyo inasababisha kupambana vyema na magonjwa nyemelezi ya kichwa kama vile mba, vidonda, kuwashwa nk.
🧚🏻‍♂️Inasaidia kuondoa infections mbalimbali kwenye kichwa kama zilikuepo na pia kulinda ngozi ya kichwa isipate infections kama haijawahi kupata.
🧚🏻‍♂️Kusaidia nywele kukua kirahisi na kiharaka zaidi, hata kama nywele zKo zilikua hazikui vizuri tumia muarobaini mara kwa mara utaona matokeo yake.

NB: Unaweza kupaka kwenye scalp tu au hata juu (kwenye nywele zote) ina nutrients za kutosha kunourish nywele zako vyema
Pia muarobaini una harufu kali kidogo hivyo kulingana na ulivyo unaweza chagua utumie kama leave in conditioner au kama steaming.

KAMA LEAVE IN CONDITIONER: 
-Unachukua majani kadhaa ya muarobaini, unayasafisha vizuri na kuyaweka kwenye sufuria
-Ongeza maji kiasi kama robo lita tu
-Acha ichemke kwa dakika 5 hivi ikiwa imefunikwa
-Baada ya hapo weka kando yapoe vizuri
-Halafu weka kwenye spray bottle yako, ongeza na mafuta kidogo kisha utakua unaspray kila ukihisi nywele kavu (wakati unataka kuzipa nywele unyevu)

KAMA STEAMING:
-Chukua majani kadhaa yasafishe vizuri
—Baada ya hapo weka kwenye blender ongeza na maji kisogo halafu saga
—Ukishasaga toa kwenye blender chuja na upate maji maji ya kijani
—Ongeza asali na mafuta yoyote ya nywele (Carrieer oils - mafuta ya mnyonyo, olive oil, coconut oil)
-—Nywele zikiwa safi paka mchanganyiko wako kwwnye nywele
—Unaweza  kucaa mfuko wa plastic, shower cap au ateamer kwa dk 30 hadi saa 1
—Baada ya hapo osha nywelw zako vizuri ili kuendelea na process nyingine kama vile LOC Method
-