HATUA ZA KUFUATA KUANZIA PREPOO HADI KUSUKA AU KUBANA STYLE
1.PREPOO (PRE-SHAMPOO)
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo inafanyika siku moja kabla ya kuosha nywele; Mfano unachagua siku maalumu ya kuosha nywel nywele zako ambayo ni Jumamosi, basi siku ya Ijumaa unafanya PREPOO ikiwa na maana ya napaka mafuta katika ngozi ya kichwa halafu una massage vizuri, na kama hujasuka unafunga mabutu au kusuka twists kisha unavaa kofia ya satini unalala. Kesho yake (siku ya pili ambapo kwa case hii ni Jumamosi) unafanya matayarsho ya HAIR TREAMENT (Hapa itaelezewa Hair treatment ambayo ni PROTEIN TREATMENT).
Mahitaji
🌿Parachichi (avocado) nusu (1/2)
🌿Asali kijiko kimoja
🌿Yai moja
🌿Mafuta kijiko kimoja( Black Castor Oil(Mafuta ya mnyonyo)/Olive oil(Mafuta ya mzeituni/Coconut oil(Mafuta ya nazi)
🌿Mayonisse kijiko kimoja
Jinsi ya kuandaa na kuchanganya
🧚♀️Changanya vitu hivyo vyote halafu unasaga kwa blender
🧚♀️Baada ya kupata mchanganyiko mzuri unaviacha pembeni
🧚♀️Unaandaa nywele zako kwa ajili ya kuosha
🧚♀️Kama ulikua hujafumua nywele zako unafumua na kufanya detangling vizuri
🧚♀️ Unachukua shampoo (sulfate, paraben and salt free) unapaka katika ngoz na kujimwagia maji kdogo kichwani
🧚♀️Baada ya hapo unaanza kusugua sugua vzuri hadi ukiridhika unasuuza vizuri
🧚♀️Kama nywele zimekatika basi unaxisuuza vzur, halaf unachukua CONDITIONER halafu napaka katika nywele zote sugua sugua kichwa kizima.
🧚♀️Unaacha kama dk 5 ivi halafu unaosha na maji safi tuu
🧚♀️ Sasa unachukua HAIR TREATMENT yako unapaka ,halafu navaa shower cap au deep conditioner cap.
🧚♀️ Kaa nayo kwa dk 35 huku unaendelea na kazi nyingine while nywele znaiva😊
🧚♀️Muda ukifika osha sasa na maji baridi or vuguvugu lakini usijmwagie maji moto sio mazuri kwa nywele.
🧚♀️Baada ya kusuuza unachukua tshirt au microfiber towel na kuanza kukausha
NB: Usitumie TAULO kukaushia nywele linakata nywele mno.
LOC Method
LOC method means Leave in conditioner, Oils na Cream
Jinsi ya kufanya
🌿Baada ya kufuta nywele unachukua leave in conditioner na kupaka nywele zote.
🌿Ukimaliza hapo unapaka mafuta ya maji (ya kimiminika)
🌿Baada ya hapo unapaka Cream ya Shea Butter unakua umemaliza
🍀Unaweza kwenda kusuka au kustyle nywele unavopenda wewe
☘️Unashauriwa usisuke nywele zkiwa kavu na wala usichane nywele kavu maana unazikosesha nywele uhai na zitakatika..
Post a Comment
Post a Comment