🍍Ushawahi kuwa na nywele ngumu haina flow, movement wala kuvutika yaani ipo ipo tu inakatika?


🍍 Afya ya nywele haitegemei tu kutumia bidhaa zilizo balance kwa PH, kubalance pia elasticity ya nywele inasaidia nywele kuwa na afya. 


🍍Nywele imeundwa kwa protein yaani keratin kwa hiyo protein inapozidi nywele inakua ngumu na inapopungua nywele inakuwa weak. So kubalance protein kutapelekea pia kubalance elasticity ya nywele vinategemeana. 


🍍Inapokuja swala la elasticity, hizi levels zinatumika kudescribe  kiwango elasticity kwa nywele yako:


🍍High Elasticity - Unapoivuta nywele yako lakini isi bounce back yani kujirudisha katika hali yake ya kuwa straight. Hii inaweza kuwa dalili ya nywele kuwa  na moisture sana na protein kuwa kidogo.


🍍Normal Elasticity - Hapa nywele inajivuta na kujirudi katika hali yake straight away. Hii ni dalili njema ya nywele kuwa na afya. 


🍍Low elasticity - Nywele inavutika na kukatika badala ya kujirudi katika hali yake. Hii ni dalili kuwa nywele ina protein nyingi na haina moisture ya kutosha. 


🍍Kwa hiyo njia nzuri ya kuensure elasticity ya nywele ni kubalance moisture na protein. Bila hivyo nywele yenye afya utaisikia kwa jirani tu😀


Je upo katika level gani ya elasticity?