Nywele natural (ambazo hazijawekwa relaxer/dawa za nywele zikiwa fupi au ndefu kama zinatunzwa vizuri huwa zinavutia sana hata ukinyoa au kuzitengeneza kwa style itakayoendana na kichwa chako.
Kutunza nywele natural na zilizowekwa dawa ni vitu viwili tofauti, hivyo ni muhimu kuzingatia mambo kadhaa ukutaka nywele zako zisizo na dawa ziwe katika ubora unaotakiwa.
🧚🏻♀️MAFUTA
Tumia mafuta ya maji kama vile ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil. Mafuta hayo ni mazuri sana kwa nywele natural kwa sababu hulainisha ngozi ya kichwa na hivyo kufanya nywele ziwe laini, zisikatike kirahisi na kuzuia mba pia. Unapotumia mafuta ya mgando kwa nywele natural ni rahisi sana kupata mba tofauti na nywele zenye dawa.
🧚🏻♀️KUOSHA
-Unapoosha nywele ni vizuri kutumia shampoo ambayo haina viambata sumu na imetengenezwa maalum kwa ajili ya natural hair. -Endapo utatumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele zenye dawa jaribu kutumia shampoo yenye conditioner; hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuosha.
🧚🏻♀️STEAMING
-Fanya steaming kwenye nywele zako angalau mara mbili kwa mwezi
-Tumia steamings zilizotengenezwa kwa ajili ya natural hair
-Fanya steamings zenye yai ni nzuri sana kurutubisha nywele za asili (Tutaielezea somo linalofuata)
-Osha nywele zako na maji ya vuguvugu kabla ya kupaka shampoo.
-Baada ya kuosha/kupaka steaming suuza na maji ya baridi; hii inasaidia kufunga cuticles.
🧚🏻♀️KUCHANA
-Nywele za kiafrika ambazo hazijawekwa dawa zina asili yabkujisokota au nyingine ni kipilipili hivyo mara nyingi zinajifunga.
-Unatakiwa kuwa muangalifu wakati wa kuchana ili zisikatike.
-Detangle nywele zako/hapa unakua unachana nywele na vidole
-Tumia chanuo pana
-Paka hair moisturizer kwenye nywele pamoja na mafuta ndio uanze kuchana taratibu
-Wakati wa kulala suka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota.
Post a Comment
Post a Comment