Leo katika somo letu la urembo ningependa kuangalia katika utunzaji wa nywele bila ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kemikali ambayo yamesababisha kwa kiwango kikubwa matatizo katika ukuaji wa nywele kama nywele kukatika,kunyonyoka,kupooza katika ukuaji n.k

Hinw ni moja kati ya mimemq ambayo watu wengi hasa wanawake huitumia katika kujiremba hasa kujichora bila kutambua kuwa mmea huo unaweza tumika katika utunzaji wa nywele zao kwa kasi kubwa. Leo tutaangalia jinsi ya kutumia hina katika utunzaji wa nywele.

MAHITAJI
•Hina vijiko vitatu vya chakula
•Kipande cha ndimu au limao
•Maji ya chai kiasi kidogo
•Gloves mbili mpya

JINSI YA KUANDAA
Vaa gloves ili mikono yako isiharibiwe na hina
•Changanya hina na viungo vingine vyote hakikisha haiwi nyepesi sana wala nzito sana
•Gawa nywele zako katika mafungumanne, kisha paka hina yako kwa uangalifu, hakikisha kila fungu limekolea vizuri na usichafue uso wako
•Baada ya hapo unakaa nayo ukiwa umevaa mfuko wa plastic au kofia ya kulalia kwa muda usiopungua lisaa
•Zikiwa tayari unaosha nywele zako vizuri na kukausha kwa kitambaa cha cotton au tshirt
•Baada ya hapo unaweza kuziweka nywele zako katika mtindi wowote ule unaopenda baada ya kupaka mafuta mazuri yasiyo na chemicals (Black castor oil, jojoba oil, coconut oil or olive oil)

ITAENDELEA...
-Matumizi mbali mbali ya hina, kama vile kung’arisha nywele, kama stemaing, kukuza na kujaza nywele nk