SABABU ZA NYWELE KUKATIKA
-Matunzo duni
Hii ni pamoja na kukaa na nywele chafu, zenye vumbi au mba na kutozisafisha mara kwa mara.
-Kutumia chanuo au kitana chenye ncha kali
-Matumizi ya drier au moto mara kwa mara kukausha nywele zako.
-Stress/ Msongo wa mawazo
-Mabadiliko ya hormones hasa kwa wanawake waliojifungua, wanaonyonyesha, wanaotumia vidonge vya uzazi mpango na wale wenye umri mkubwa (waliofikia menopause stage).
-Ukosefu wa protein ya kutosha (kwenye mlo pamoja na kwenye steamings).
-Ujauzito ambao hupelekea mtu kuwa na stress ambapo wengi baada ya kujifungua tatzo huwa linaisha.
-Anaemia
SULUHISHO LA MATATIZO HAYO
-Muone daktari kwa matatizo ya stress (kisaikolojia)
-Tumia shampoo yenye virutubisho vya asili, isiyo na viambata sumu kama vile paraben, chumvi na sulphates.
-Hakikisha unapata mlo kamili (Chakula chenye virutubisho vyote ambavyo huchangia katika ukuaji wa nywele).
-Kunywa maji mengi na pata muda wa kutosha kupumzika.
NJIA MOJAWAPO UNAYOWEZA KUTUMIA KUPUNGUZA TATZO HILO
Hii inatumika kwa nywele za asili tu (ambazo hazina dawa).
MAHITAJI
🧚🏻♂️Tangawizi vipande 3
🧚🏻♂️Mafuta vijiko viwili
🧚🏻♂️Maji robo lita
JINSI YA KUTUMIA
-Chukua tangawizi isage ilainike vizuri
-Weka maji robo lita pamoja na mafuta ,hakikisha tangawizi iliyosagwa imechanganyika vizuri na maji yako .
-Chuja vizuri ,kisha paka kichwani hakikisha unapaka hadi kwenye ngozi ya kichwa..
-Vaa kofia ya plastic kwa saa 1 au zaidi
-Osha nywele zako vizuri kwa shampoo
-Tumia mara moja kwa wiki 2 kwa matokeo mazuri zaidi.
NB: Njia hii inazifanya nywele zako ziwe imara, nyeusi na ndefu zaidi.
Post a Comment
Post a Comment