Hili ni swali ambalo watu wengi wenye nywele zenye dawa wamekua wakiuliza; Je nifanye nini ili nywele zangu ziwe za asili?. Leo tuangalie njia kuu mbili ambaxo unaweza kutumia ili kurudi kuwa natural (kuacha kabisa kutumia dawa ya nywele). Pia tutaangalia na hasara na hasara ya kila njia maana faida yake zote in general ni kupata nywele natural.
NJIA YA KWANZA
1.TRANSITION METHOD
Hiki ni kitendo cha kuacha dawa / matumizi ya dawa za nywele na kuruhusu ikue yenyewe huku ukikata (au kutrim) kidogo kidogo nywele za juu mpaka utakapimaliza nywele zote zenye dawa.
FAIDA YA TRANSITION
🧚♀️Unapata muda wa kuisoma nywele yako vizuri
🧚♀️Kama haupo huru na nywele fupi unabaki na nywele zako ndefu
🧚♀️Hausubiri kukua kwa nywele
🧚♀️Wakati wa transition unamuda wa kustyle na kusuka nywele zako upendavyo
HASARA ZA TRANSITION
🧚♀️Texture ya nywele inakua tofauti
🧚♀️Process ya transition inachukua muda mrefu kuliko kuzikata kabisa
🧚♀️ Nywele kukatika ni lazima na huwezi kueluka; Kwani nywele yenye dawa zina heat na chemical damage hivyo ni lazima zitoke tu.
VITU VYA KUZINGATIA KIPINDI HIKI
🧚♀️Katika kipindi hiki ni lazima KUEPUKA na wala KUJARIBU kutumia moto hotcombs na blow dryers vile vile usipige pasi nywele zako utaharibu za chini zinazopelekwa kuwa natural.
🧚♀️Acha kabisa kutumia bidhaa zenye viambata sumu especially SULFATES NA PARABENS 🧚♀️PROTECTIVE style; Fanya protective style kupunguza manyanyaso ya kila siku kwako personally (maumivu ya kuchana nywele na kuzitreat) pia kwa nywele kusumbuliwa sumbuliwa kila siku. Protective style ni mitindo ambayo unaweza kufanya na kukaa nayo atleast siku 5 au zaid bila kuchana.
🧚♀️ kumoisturize (kuzipa unyevu) nywele zako
🧚♀️ TRIM ncha mbovu mara kwa mara vizuri zaidi ni baada ya miezi 2 au zaid ili kuondoa split ends (ncha zilizochoka) - Unatumia mkasi ila sio wa nguo.
NB: Pale nywele za asili zinaporefuka na kukutana na za dawa ndipo kazi itaanza maana Hii sehemu huwa ni dhaifu sana Jitahid kufanya deep conditioner (steaming kwa lugha iliyozoeleka) kila wiki ili kulinda na kuzipa nguvu nywele.
NJIA YA PILI
2. BIG CHOP (BC)
Hii ni kwa wale wanaotaka kuwa na nywele natural kuanzia mwanzo sasa wanakata nywele zote za dawa na kubaki na nywele vifupi - TWA (teeny weeny Afro). In general in KUNYOA tu.
FAIDA ZA BIG CHOP
🧚♀️Hausubiri muda mrefu kuanza kuzitunza nywele zako kiusahihi
🧚♀️Unaanza fresh kabisa bila dawa
🧚♀️Unakua na uwezo wa kujua aina ya nywele zako haraka na hivyo itakua rahisi kuzihudumia.
HASARA ZA BIG CHOP
🧚♀️Unasubiri kidogo ili nywele zikue
🧚♀️Unatakiwa uitambue nywele yako haraka
🧚♀️Inaanza na style mpya ya kuwa na nywele fupi.
BUT: Yote ni maamuzi yako angalia ipi itakua njia sahihi kwako.
La muhimu zakdi ni KUEPUKA MATUMIZ YA MOTO WA AINA YOYOTE ILE KWENYE NYWELE.
Post a Comment
Post a Comment