NJIA YA  PILI
🧚‍♀️Chukua nazi iliyokomaa vizuri (sio zile  changa)
🧚‍♀️Kuna  nazi vizuri  kwa kutumia njia yeyote iliyo rahisi kwako  kama una mbuzi,
food processor, blender, grater au grapefruit spoon yoyote unaweza kutumia.
🧚‍♀️Chukua  maji ya vuguvugu kiasi kisha ongeza kwenye ile nazi uliyokuna
🧚‍♀️ Changanya na mikono yako kwa dakika 1 hadi 2
🧚‍♀️Kamua vizuri kwa kutumia chujio la nazi au cheese cloth ili upate tui la nazi.
🧚‍♀️Unaweza kurudia mara kadhaa kuweka maji ya vuguvugu ili kutoa matui yenye mafuta yote (mafuta yote kwenye nazi in general).
🧚‍♀️Ukishapata  tui  weka katika chupa na liache likae kwa  masaa 24 ili mafuta yajitenge na maji.
 🧚‍♀️Au unaweza weka jikoni (medium heat) kwa muda wa saa moja au mpaka maji yameondoka na yaliyobakia ni mafuta tu (au kwa kiwango kikubwa)
🧚‍♀️ Toa mapovu ya juu halafu weka mafuta yako katika chupa utakayoandaa.
🧚‍♀️Hadi hapo mafuta yako yapo tayari kutumia.

ITAENDELEA NJIA YA TATU❤️