Hii ni hatua muhimu sana katika ukuaji na utunzaji wa nywele. Uchanaji sahihi wa nywele  unaweza kuzipa nywe zako  hadhi ya kuwa na muonekano mzuri, kukua  vizuri, kuzuia kukatika na kupunguza au kutoa maumivu kabisa wakati wa kuchana nywele (hasa wenye nywele asilia au kipilipili - 4C hair type). Leo nitaelezea njia sahihi ya kuchana nywele zako kiusahihi zaidi.

MAHITAJI
🧚🏻‍♂️Chanuo kubwa
🧚🏻‍♂️Spray bottle yenye maji
🧚🏻‍♂️Mafuta ya kimiminika (Mafuta ya nazi/Olive oil/Black castor oil-au waweza changanya yote kwa viwango sawa sawa)
🧚🏻‍♂️Leave in conditioner (Ya chaguo lako-nzuri zaidi ni za Auntie Jackies au Cantu products)
🧚🏻‍♂️Applicator bottle

JINSI YA KUFANYA
🍃Weka maji kwenye spray bottle
🍃Ongeza leave in conditioner kidogo
🍃Ongeza mafuta kidogo pia kisha tikisa vizuri mchanganyiko wako
🍃Spray  mchanganyiko wako katika nywele kiasi sio sana
NB: Tunaspray  huo mchanganyiko kwa sababu inasaidia kuongeza unyevu (moisture) na kurahisisha kuchana kucha nywele maana haitakiwi kuchana nywele zikiwa kavu. Kwa kuwa ukichana nywele kavu ni rahisi kukatika.
🍃Baada ya hapo tumia  vidole vyako kukata nywele mafungu, kuanzia mafungu 4 hadi 6 kulingana na nywele zako kama ndefu au fupi
🍃Chana kwa kutumia vidole  huku ukichambua mpaka uone nywele zimechambuka vizuri na hazijajifunga kwa kuwa 4 type hair  (ambazo waafrica wengi wanazo)  asili yake kujifunga hii inaitwa finger detangle husaidia kutoa nywele zilizojifunga.
🍃 Chukua kitana kikubwa,chana kuanzia juu ya nywele kuja chini taratibu
🍃Then unaweza kutwist,au kusuka mabutu au tumia kibanio kubana nyweke zilizochanika vizur then unahamia fungu lingine mpaka utakapomaliza zote

Hii ina faida nyingi sana kama vile;
🍃Inasaidia kutokata nywele wala kutoumia wakati wa kuchana sababu nywele zinakuwa na unyevu wa kutosha halafu  zimechambuka vizuri.

Pia unashauriwa unapoweka deep conditioner (steaming kwa lugha iliyozoeleka) hakikisha umechana nywele zako vizuri ili kufanya nywele zilainike na steaming iziguse au izifikie nywele zote.