TOFAUTI KATI YA MBA (DANDRUFF) NA NGOZI KAVU (DRY SCALP)
Mba/dandruff unasababishwa na mafuta mengi kwenye nywele (sebum) hasa ya mgando n.k (zipo kwenye somo la mba No. 24) lakini Ngozi kavu (dry scalp) ni ile hali ya ngozi kutokua na unyevu unyevu na inasababishwa na kutokuipa ngozi yako ya kichwa unyevu wa kutosha na muda inapotakiwa.

UTAJUAJE KAMA UNA MBA AU NGOZI KAVU?
Mba unaonekana kabisa kama particles ndogo ndogo (unaonekana kabisa kwa macho) na muda mwingine hadi vidonda lakini ukavu wa ngozi unaweza kusense kwa kushika na kunakua kama imepasuka na hii husababisha nywele zisikue au kudumaa LAKINI vyote viwili vinatambulishwa kwa;
-ngozi ya kichwa kuuma au kuwasha
-unaweza kuwa huna mba ila unawashwa (hiyo ni ukavu wa scalp)

UKAVU WA NGOZI YA KICHWA
Kwanza inafaa ufahamu ni nini kinacho kusababishia nywele zako kuwa kavu , na kuanza kukatika katika, mara nyingi nywele kuwa kavu inaweza kutokana na sababu mbalimbali. Hapa kuna machache, na kipi unachoweza kufanya ili kurejesha unyevu katika nywele zako kavu:

VISABABISHI VYA UKAVU KWENYE NGOZI YA KICHWA
☘kutumia vifaa vyenye joto kali kukaushia nywele (hair dryers) , vinaweza kusababisha nywele kuwa kavu.
☘Kuosha nweyele zako mara kwa mara kwa shampoo (Overwashing) bila kuwa na tahadhari kama vile kutumia leave in conditioners na conditioners.
☘kuachia nywele zako kwa muda mrefu kwenye mwanga wa jua,upepo
☘kutumia maji ya chumvi kwa muda mrefu kuosha nywele zako kunaweza kusababisha ukavu wa nywele pia.
☘kutumia chemicals hatari kwa nywele (viambata sumu) mara kwa mara husababisha nywele kuwa kavu.
☘kutumia brash mbaya au styles mbaya ya uchanaji nywele pia husababisha kupoteza unyevunyevu wa nywele na hivyo kufanya nywele kuwa kavu.
☘kutokuficha ncha kwenye mitindo ya nywele

NINI  CHA KUFANYA KUKINGA NYWELE ZAKO ZISIWE KAVU
☘Usitumie shampoo kila mara kuosha nywele zako, kila kitu kizuri ukikitumia kwa wingi kupita kiasi kinakua na madhara hapa jaribu kupangilia angalau siku mbili mbili au zaidi maan hata kutumia shampoo kwa wingi zaidi ina leta madhara, kitaalamu inashauriwa osha nywele zako co-wash angalau mara mbili kwa mwezi na mara mbili hadi tatu kwa mwezi kwa kutumia shampoo
☘Tumia shampoo nzuri inayoendana na nywele zako, hapa yakupasa utambue una aina gani ya nywele na je, ni shampoo ipi ianakufaa zaidi? usitegemee shampoo za saloon ni vyema hata ukienda saloon ukaenda na shampoo yako mkononi kwani saloon nyingine hata shampoo wanachanganya na maji, usiende tu saloon ukakubali kuoshwa hata kwa shampoo usizozifahamu nyingine sio shampoo kabisa
☘Vaa kofia laini au kitambaa ulalapo, jenga mazoea ya kuvaa kofia laini ya kulalia ili kutunza unyevu nyevu wa nywele zako unapolala bila kuwa na kofia au kitambaa unaweza usababisha nywele kuvurugika na wakati mwingine hupoteza unyevu wake taratibu na huweza kusababisha kuwa na ukavu
☘Punguza mionzi ya kunyooshea nywele zako, siku ukitaka kubadili muonekano au ur hair style ukaamua kuzichoma/kusipasi au kunyoosha nywele zako kwa kutumia moto au umeme…unashauriwa kupunguza temperature au kutumia kinga (mafuta maalum) ambayo inafanya nywele zako zisipate damage wakati ya kuzinyoosha hii itakusaidia kutunza moisture sambamba na kupunguza ukatikaji wa nywele zako
☘Tumia Moisturizer/Vilainishi Vya Nywele mara kwa mara, Hakikisha unatumia moisturizer kila siku Wengine hawafanyi kila siku. Inategemea na aina za nywele ulizonazo. Wakati wa kuweka moisturizer,hakikisha unapaka kila mahali haswa kwenye ncha za nywele zako(split ends). Mara nyingi huwa tunazisahau zile za juu. Badala yake wengi tunapaka zaidi kwenye ngozi ya kichwa tu. Ndio maana huwa inasisitizwa kuzikata zile split ends kwa sababu huwa zimekauka na kuwa dhaifu.