Unaweza kua na ngozi laini sana kwenye uso wako au mwili kwako lakini linapokuja swala la viwiko vya mikono/elbows au magoti case inakuta tofauti sana sababu unakuta kunakua na weusi,roughness na hata kua na vipele au unakuta pamebabuka/ngozi kutoka toka ,simply sio palaini.
Haya ni matatizo ya kila siku na wanawake wengi ni swala linalotukumba wengi wetu.Wengine hadi kufikia kuficha sehem hizi za mwili sababu zinawa aibisha au...
wanaona aibu kuzionyesha .
Kama na wewe ni muhanga basi nakupa baadhi ya tips tena home remedies ambazo zinatoka jikoni kwako ili kukusaidia kufanya ngozi hizi za sehem mbili kuna na unafuu na kumaliza tatizo.
Kwanza tujue kwamba matatizo haya ya ngozi kua rough na nyeusi kwenye magoti na viwiko vya mikono inasababishwa na nini???
🌸Sehemu hizi zinaukosefu wa glands za mafuta kitu kinachopelekea ziwe kavu haraka na hadi kua nyeusi kuliko kawaida.
🌸Mara nyingi wengi wetu hizi sehem huwa wala hatuzijali ,tunaziacha zenyewe unakuta ile layer ya ngozi iliyokufa haiondolewi inakaa tu na kufanya pawe pagumu na pakavu.
🌸Kingine mkusanyiko wa dead cells kwenye sehem hizi kunasababisha kuwe rough na ile layer inatakiwa kuwa inaondolewa mara kwa mara ili ku renew ile ngozi.
NINI KIFANYIKE KUONDOA UGUMU HUO
☘️Scrub ya sukari
Scrub inasaidia kupeel/kuondoa cells zilizokufa ambazo zinasaidia cell mpya kutengenezwa na kufanya ngozi kuonekana nzuri na soft.
Kutengeneza scrub hii unahitaji
Changanya Kijiko kimoja cha Asali na sukari ya kawaida ,pakaa/sugulia kwenye goti lako au viwiko vya mikono kwa mwendo wa duara ,Ile sukari itasaidia kutoa ile ngozi ambayo haitakiwi,then osha na maji safi ,unatakiwa kufanya hizi kwa wiki mara moja.
☘️Limao na juice ya viazi ulaya
Viazi ulaya (mviringo) na limao zina properties za bleach which inazifanya ziwe chaguo la wengi kwenye mambo ya urembo.
Hapa unakata limao nusu sugulia kwenye elbows/knees au kata pia kipande cha kiazi mviringo na ufanya the same Kama limao ,hii itasaidia kufanya ngozi hii iwe lighter .Then tumia Asali ambayo itasaidia ku moisturize ngozi yako pia.
☘️Oil massage
Mafuta yanaingia kwenye ngozi na kusaidia ku moisturize naturally na internallu ,sababu hizi sehem hazina oil glands kwa kuzi masage na mafuta mara kwa mara na olive ,almond au coconut oil/mafuta ya nazi,kutasaidia pia pa shine ,So massage na mafuta moja wapo kati ya hapo na acha usioshe mafuta yaingie vyema kwenye ngozi.
☘️Tumia dodoki au Jiwe lile laini
ukioga waweza tumia jiwe laini au dodoki kusugua sehem za magori na viwiko vya mikono,usisugue kwa nguvu just be gentle ,itasaidia ku exfoliate ngozi ayako ,si lazima kufanya kila siku unaweza pata vidonda na ukiwa unasugua fanya kwa circular motion.
☘️Moisturizer
Chukua mafuta yako paka kwenye ngozi ili kusaidia paendelee kua soft ,baada ya hizo remedies zote ukishafanya hakikisha huachi magoti yako na elbow bila kupaka mafuta hii itasaidia pasiwe pakavu na rough.
Post a Comment
Post a Comment