Kwa wale ambao tuna nywele asilia ( natural hair) tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.

Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri? Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka na kupenda nini?

KARIBU UJIFUNZE

- Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh.. nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri hivyo jambo la msingi la kuzingatia katika nywele zako ni kujenga mahusiano mazuri tu na nywele zako ,zielewe, ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

- Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele. Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri. Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki(Products zisizo na viambata sumu). Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi. Unapoziacha chafu, ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia, kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

-Linda unyevu wa nywele zako
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji. Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu. Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu. Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri, na zikikauka zinakua kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri, ukazi-’condition’. Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache, pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

- Zifahamu nywele zako
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu. Unajuaje?
Nilishaelezea kwenye posts zilizopita ila leo pia nitarudia kwa kifupi..
🧚‍♀️Chukua kikombe,kijaze maji safi (Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi)
🧚‍♀️Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.
🧚‍♀️Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.
MATOKEO
-Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.
-Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida .(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)
Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

🧚‍♀️Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.
🧚‍♀️Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.

Je wewe una nywele aina gani? Tukutane kwenye comments😘

KUMBUKA: NYWELE NZURI NI MATUNZO NA HAKUNA NYWELE ZINAZOKATAA MATUNZO MAZURI

ITAENDELEA....