Ni kwa muda sasa tumekua tukiongelea jinsi ya kulainisha nywele, kufanya ziwe nyingi nk; Leo tuangalie jinsi ya kufanya nywele ziwe nyingi (kuongeza volume) , kuwa nyeusi na zipendeze kwa kutumia vitu vya asili kabisa unavyoweza kuvipata ukiwa nyumbani.
SABABU ZA KUWA NA NYWELE NYEKUNDU NA NYEPESI
🧚🏻♂️ Kupaka paka madawa nywele; Hii hupoteza rangi halisi ya nywele ambapo wengine huwa na nywele nyekundu hata kama zilikuwa nyeusi.
🧚🏻♂️Kutumia moto mara kwa mara kama vile kublowdry, kupasi na kunyoosha nywele kwa kutumia moto.
Katika mazingira hayo unaweza kutumia vifuatavyo ili kurudisha volume na rangi halisi ya nywele.
🧚🏻♂️Baking soda: Hii inatumika baada ya kusafisha nywele zako na kuwa safi.
JINSI YA KUANDAA
🍃Pima vijiko vitatu vya chai (vile vidogo) vya baking soda
🍃 Unachanganya na maji
🍃 Unachanganya vizuri mchanganyiko wako na unatumia kuoshea au kusuuzia nywele.
Hii inasaidia sana katika kuleta rangi halisi ya nywele.
🧚🏻♂️Asali na mafuta ya mzeituni (Olive oil): Hii inasaidia kwa wale ambao wana tatizo la muwasho au kupata tatizo lolote kichwani huenda nywele zinakatika bila wewe kujua, tumia vitu hivyo vitakuweka sawa.
JINSI YA KUANDAA
🍃Chukua asali vijiko viwili (au utakayoona inatosha)
🍃Pima na mafuta ya mzeituni nusu kikombe.
🍃Changanya vizuri mchanganyiko wako
🍃Paka vizuri kwenye eneo lenye tatizo
🍃Unaweza kuvaa shower cap au ukaacha ivo ivo
🍃Acha kwa kwa muda wa dakika 20 hadi 30
🍃Then osha kwa maji ya baridi.
Nikisema sehemu yenye tatizo namaanisha kama nywele zimepukutika au una mba wanaosababisha unajikuna sana nk.
🧚🏻♂️Papai: Hili linasaidia kwa watu wengi maana wakishaweka dawa kichwani huwa wana tabia ya kutaka kuzikata ili wazilinganishe huko saloon, lakini steaming hii ya papai ambayo unaweza kuifanya nyumbani kwako ina uwezo wa kuzifanya nywele zako zilingane.
JINSI YA KUANDAA
🍃 Chukua yogurt kiasi
🍃 Papai nusu,
🍃Vichanganye kwa pamoja (au blend kiurahisi zaidi)
🍃 Kisha baada ya hapo paka mchanganyiko huo kwenye nywele zako
🍃Vaa shower cap au steaming cap
🍃Acha kwa muda wa nusu saa
🍃 Osha kwa maji ya vuguvugu.
Nywele ndefu kwa ujumla: kuwa na nywele ndefu
🍃Chukua yai moja
🍃Mafuta ya mnyonyo (Black castor oil) vijiko vitatu
🍃Kijiko kimoja cha Vinegar
Changanya kwa pamoja kisha paka nywele zako acha kwa muda wa dakika 30 kisha osha.
Post a Comment
Post a Comment